Pages

Tuesday, February 12, 2013

Mke wa Mwanamuziki Jose Chameleone, Daniella Atim amejikuta ameangukia mikononi mwa sheria baada ya kufunguliwa mashtaka kwa kumshambulia na kumpiga kofi mwandishi wa habari ambaye amefahamika kwa jina la Kuku Wazabanga huko Uganda.

Kuku Wazabanga
Daniella
 
Daniella ametajwa kufikia hatua hii baada ya mwandishi huyu kuzua madai kuwa Nyumba ya msanii Chameleone iliyopo huko Sseguku ambayo aliihama na familia yake hivi karibuni kwa sababu za kiusalama, ipo katika hatihati ya kutaifishwa na maafisa mkopo kutokana na Deni ambalo hawajalipa.

Taarifa hizi ambazo zimeonyesha dhahiri kumuudhi Daniella, ndizo zilizosababisha apige mishe za kumtafuta mwandishi huyu na kuingia naye katika ugomvi mkubwa uliozaa tukio hili. 

Kwa sasa Daniella anakabiliwa na kesi ya kushambulia/kupigana hadharani na yupo nnje kwa dhamana ya kitita cha shilingi Milioni 20 za Uganda.

Chameleone na familia

0 maoni:

Post a Comment

Labels