Pages

Thursday, February 28, 2013

DADA YAKE GOLDIE AWEKA WAZI SABABU NYINGINE ILIYO SABABISHA KIFO CHA GOLDIE

Mdogo wake marehemu Goldie Harvey, Joshua Filani ameweka wazi kifo cha dada yake Goldie kuwa kimechangiwa na msongamano mkubwa wa foleni za magari kutokana na kwamba siku hiyo watu wengi walikuwa kwenye pilika pilika za sherehe ya siku ya wapendanao yaani Valentines Day.

Joshua ndie aliyekuwa mtu wa mwisho kuongea na marehemu dada yake wakati wakiwa pamoja kwenye gari ambapo wakati Joshua akiongea na baba yao, ghafla Goldie alimpokonya simu hiyo ya mkononi na kumwomba baba yake amsalie wakati huo akilia kutokana na kupatwa na maumivu makali ya kichwa.

Maumivu hayo yalimpelekea Goldie kulia na hatimaye kuzimia na kuingia katika hali ya kutopteza fahamu kiasi cha mdogo wake kuchanganyikiwa, ambapo walichelewa kufika haraka hospitalini hapo kutokana na foleni za magari ukizingatia watu walikuwa katika shamra shamra za kusheherekea Valentines Day.

0 maoni:

Post a Comment

Labels