Pages

Sunday, February 10, 2013

RAPPER KUTOKA MBEYA CITY 'IZZO B' AMEPATA SHAVU LA KUTENGENEZEWA NGOMA NA PRODUCER MKONGWE KATIKA MEDANI YA MUZIKI "MASTER J" WA MJ RECORDS

Rapper kutoka Mbeya City anae-hit na ngoma yake ya ''Ball Player'' akimshirikisha Ngwair, Quick Rocka na Ruth amepata shavu la kutengenezewa ngoma na Producer mkongwe katika medani ya muziki, mtu mzima Master J [MJ RECORDS] ikiwa ni kama zawadi kutoka kwa producer huyo.

Mbeya Boy aliandika katika moja ya account zake za mtandaoni akiwa amepiga picha na Producer Master J siku ya Alhamis, "Nakushukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kurekodiwa nyimbo na Master J leo tarehe 7/2/2013 siwezi sahau siku hii"  akionekana kuisubiria siku hii ambayo hatimaye imetimia.
 
Izzo Bizness amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na Master J hasa katika masuala ya kimuziki na maisha lakini toka ajiunge na label ya MJ Records mara nyingi ngoma zake zilikuwa produced na Producer Marco Chali ambae pia yupo chini studio hizo, sasa this time Master J anamsukia dundo moja kama offer kwa rapper huyo.

Go Izzo Bizness a.k.a Ball Player, dream just came true, tunasubiria that other hit kutoka kwenye mikono ya Master J himself... MBEYA CITY STAND UUUPPP!!!!

0 maoni:

Post a Comment

Labels