Pages

Wednesday, February 13, 2013

Size 8, Mwanamuziki mkali na ambaye kwa sasa nyota yake ipo juu kabisa kimuziki Afrika Mashariki, ameonesha moyo wake kipekee wa kupenda kusaidia jamii zaidi

Size 8
Size 8, Mwanamuziki mkali na ambaye kwa sasa nyota yake ipo juu kabisa kimuziki Afrika Mashariki, ameonesha moyo wake kipekee wa kupenda kusaidia jamii zaidi baada ya kuahirisha tamasha kubwa kabisa alilopanga kuzindua mtoko wake mpya ili kupata nafasi ya kushughulikia zaidi mpango wa kusambaza ujumbe wa amani unaoendelea sasa huko Kenya.

Size 8 amepeleka mbele uzinduzi huu ambao kiukweli ungempatia mpunga mrefu mpaka baada ya uchaguzi mkuu wa nchi ya Kenya, na hii ni kwa sababu sasa ameamua kuwekeza nguvu zake zote kufanya kampeni za kuzuia uwezekano wowote wa kuzuka kwa vurugu.

Shughuli anayoifanya Size 8 kwa sasa haimuingizii pesa yoyote, kitu ambacho kimetafsiriwa kuwa ni upendo na mfano mzuri kutoka kwa mtu kama yeye ambaye ni kioo cha jamii. haimuingizii pesa yoyote, kitu ambacho kimetafsiriwa kuwa ni upendo na mfano mzuri kutoka kwa mtu kama yeye ambaye ni kioo cha jamii.



Size 8
#FAHAMU pia kuwa Size 8 ambaye anabamba sana na ngoma yake ya Vidonge, pia yupo katika nafasi ya juu kabisa katika orodha ya wasanii wa kike wanaovuta 'mulla' ndefu zaidi Kenya kwaajili ya kupanda jukwaani kutumbuiza.




HABARI KWA HISANIYA:-www.sammisago.com

0 maoni:

Post a Comment

Labels