Hatimaye ile ndoa ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Nigeria, 2Face Idibia na mchumba wake Annie Macaulay Idibia sasa inatarajiwa kufungwa Tarehe 23 March mwaka huu.
Masaa machache yaliyopita, Annie aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa ndoa hiyo itafungwa Dubai.
Annie na mumewe mtarajiwa walikwenda Dubai kuangalia ukumbi ambao watakaofanyia harusi hiyo.
Baadhi ya mastar kutoka Nigeria ambao watahudhuria harusi hiyo ni Don Jazzy, D'banj, Banky W, P-Square na wengine wengi.
0 maoni:
Post a Comment