Pages

Sunday, January 20, 2013

AMAZONI AJITOA KATIKA KUNDI LA MTANASHATI ENT

         
Msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Amazon ameweka wazi kuwa amejitoa Watanashati Entertainment, kwa kile alichodai kuwa Bosi wa kundi hilo ambae ni Hustadhi Juma Na Musoma, alikuwa anataka kumpa mkataba wa milele kitu ambacho kimemfanya Amazoni aone kama ni lengo la kummaliza kimziki.
         
Amazon alisema kujitoa kwake ni kwa roho safi lakini amesikitishwa sana na Bosi huyo kutaka kumpa mkataba wa milele ambao utambana yeye kutokufanya kazi nyingine. Pia aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na hilo kwa sasa atakuwa akifanya muziki kivyake hadi pale atakapo pata meneja mpya wa kuweza kusimamia kazi zake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels