Pages

Friday, January 18, 2013

Suma Mnazaleti Kuja Na "Tuko Wangapi" Hivi Karibuni

      
Hit-Maker wa track ya Chukua Time maarufu kama Suma Mnazaleti sasa yuko mbioni kuachia ngoma yake nyingine inayokwenda kwa jina la Tuko Wangapi huku akiwa amemshirikisha Tundaman.

Suma amesema kuwa ngoma hiyo inazungumzia namna mapenzi ya uongo yalivyo huku wanawake wengi wakiwa na wanaume wengi na mwisho wa siku anaamua kuweka na kuuliza Tuko Wangapi kwa lengo la kutoa utata na kuyakimbiza matatizo yanayoweza kutokea.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa wimbo huo pia utakuwa ni fundisho kwa wanaume wengi wanaopenda kuona mwanamke na kutokujua nguo anazovaa zimetoka wapi, badala yake wanafurahi na hawajui kuwa wanaume wengi wanakula tunda. Hivyo basi, mashabiki wa Suma kaeni tayari kwa ujio mwingine kutoka kwake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels