Pages

Monday, January 28, 2013

Video Ya PRESS PLAY Kutoka Mwisho Wa Mwezi Huu...

     Hivi karibuni tuliona picha za Director Nisher kutoka Nisher Entertainment kutoka A-Town akishuka Bongo, DSM kwa ajili ya kurekodi video ya ngoma mpya ya DJ Choka a.k.a Mr. ApetitePRESS PLAY. Nisher alitua na mzigo ukafanyika, sasa mpya ni kwamba video hiyo itatoka mwisho wa mwezi huu... inayofahamika kama
    
 Ujumbe huo kuhusu video hiyo iliyomuweka Nisher hapa Bongo zaidi ya wiki, ulitoka katika uongozi wa BHitz music Group kupitia ukurasa wao wa Twitter ikiandikwa, "Press Play Video Official Release 31.1.13" yaani mwisho wa mwezi huu wa kwanza wa mwaka....
Track hiyo inayoshirikisha wasanii wakali kutoka BHitz, kama Deddy, M-Rap, Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby inataraji kudosha kichupa hicho tarehe hiyo... Tusubiri tuone.

0 maoni:

Post a Comment

Labels