Q
Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta
yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.
Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila
anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Qchilla
amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa
wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia
madawa hayo.
Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye
matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na
kuishika dini.
Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia
alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela
aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama
aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni
waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.
QChilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa
zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi
kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani
tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa
nyimbo kali.
kwa Hisani ya Clouds fm
0 maoni:
Post a Comment