Pages

Tuesday, January 22, 2013

BEN POL ATENGUA MSIMAMO WAKE WAKUTOTAKA FANYA COLLABO NA WASANII WENGINE



Kama unakumbuka vizuri mwaka jana Ben Paul alisitisha kufanya Collabo na msaani yoyote mpaka February 3, 2013, Lakini hapa katikati tumeskia Yatakwisha ft Linnah, Lord Eyes ft Ben Paul - No More Drama na Mama Yoyo Aliyoshirikishwa na G Nako.
Leo Ben Paul ametengua kaulia yake kuhusu kusitisha kufanya collabo na kusema atakuwa akifanya collabo kwenye Ngoma nzuri .
Ataangalia Potential ya Msanii ,Wimbo wenyewe na Production. Ben alisema ata International artist wanafanya collabo nyingi ila hawashuki kwa sababu wanazingatia Mambo hayo.

Kuhusu wimbo wake wa kwanza kutoka mwaka huu Ben amesema `Jikubali' Inamuhusu mtu anaye Weka Tofauti kati yake na watu wenye mafanikio, watu maarufu na ata wanasiasa. 
Hii ngoma itamuhamasisha afanye vizuri kwenye jambo analolifanya ,kama ni kazi , elimu ,sanaa au chochote. 
Huu wimbo unampa nafasi yakujiona ni mtu mwenye uwezo wakufanya kazi nzuri na akafanikiwa na kusaidi familia yake. Mtu huyo atuone sisi kama watu wa kawaida. Wimbo unatoka Kupitia Video kwanza alafu audio ndio itafata.

0 maoni:

Post a Comment

Labels