Pages

Wednesday, January 16, 2013

Nikki Mbishi Ampa Stamina Ubunge Wa Morogoro

       
Rapper kutoka MLab, Nikki Mbishi hivi karibuni alimpa rapper mwenzie Stamina, ubunge wa Morogoro kwa kumfananisha na Mh. Joseph Mbilinyi [SUGU] ambae ni mbunge wa Mbeya Mjini

Nikki Mbishi aliyasema haya hasa kwa kuonekana kukubali anachofanya Stamina kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, na kuandika "Stamina is our new SUGU, mbunge wa Morogoro".

      
Hii ni heshima kubwa sana aliyompa Stamina hasa kwa kumfananisha na SUGU, hasa ukizingatia Nikki Mbishi ni msanii mkubwa kuliko Stamina

Hii inaonesha ni jinsi gani Nikki Mbishi anamkubali rapper huyu from Moro Town, Well hii ni nzuri, hasa wasanii kwa wasanii wanapoonekana kusikiliza, kutambua, na kukubali kazi zinazoendelea kwenye industry hii ya muziki wetu.
       
Stamina ni msanii anaefanya miondoko ya Hip-Hop [Kama ilivyo kwa Nikki Mbishi] mwenye chimbuko la Morogoro anaefanya vizuri sana katika muziki huo hapa Tanzania. Punchlines, Bars, Mashairi n.k. ni baadhi ya vitu anavyovimiliki rapper huyu. Kwa sasa, Stamina anatamba na track yake mpya ya WAZO LA LEO akiwa amemshirikisha Fid Q na anatarajia kuachia album yake mpya yenye tracks 22 hivi karibuni.

0 maoni:

Post a Comment

Labels