Pages

Tuesday, January 22, 2013

Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.


Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.

Izzo amesema ameamua kubadilisha style kidogo kwani ingekuwa ni  marudio ya kazi alizozifanya mwaka jana .

Wimbo unatoka kesho na WaTanzania ndio wataamua kama ni ujio mzuri wa Izzo au Akajipange tena .

Kwenye wimbo huu ataskika kwa mara ya Kwanza Msanii Ruth aliyefanya Chorus,Izzo amesema kuwa beat ya Ball Player imetengenezwa na Nahreel huku vocal na final mixing ikafanywa na Lamar wa Fish Crub.

Amesema wazo la kuja na wimbo wenye jina la ‘Ball Player’ ni kulinganisha juhudi za mchezaji mpira awapo uwanjani ambaye huwa na pilila pilika muda wote na jinsi ya kutumia mfano huo katika maisha ya kawaida. 

Amejitolea mfano yeye wakati anakuja Dar es Salaam kutokea Mbeya alifikia kwa washkaji lakini kwa sasa anaishi kwake mwenyewe kutokana na juhudi zake katika kutafuta maisha.

0 maoni:

Post a Comment

Labels