Pages

Thursday, January 10, 2013

FAHAMU KUHUSU NDOA YA TIMBULO NA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE.


Msanii wa Bongo Fleva Ally Timbulo amekaririwa  akisema Album yake ipo tayari na inatarajiwa kutoka mwaka huu na itakuwa na nyimbo 10 zikiwemo, Bado Kijana ,Domo langu ,Waleo wa Kesho na Samson na Delilah .

 Pia ule wimbo aliofanya na kundi la X- Maleya 'Lastic Ya Upendo' kutoka Cameroon Utakuwepo Kwenye Album Hio.  Kuhusu Jina la album ,Timbulo amefunguka nakusema  Kwa sababu Wimbo wake wa Kwanza na Ulio mtambulisha Ni Domo Langu basi Domo Langu Ndio Jina la Album.
  
Kuhusu kutangaza Ndoa Jana ,Timbulo amesema ni mpango wa Mwaka 2013 na anaufanyia kazi ,siku yoyote mwaka huu atamtangaza mchumba wake rasmi. Anamuomba Mungu amuonyeshe Njia sahihi ya kufanya mambo yake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels