Pages

Monday, March 11, 2013

2FACE APEWA ZAWADI YA GARI MBILI NA GAVANA WAJIMBO LA IBOM HUKO NIGERIA

Mheshimiwa Godswill Akpabio
Kitendo cha gavana wa jimbo Akwa Ibom huko Naijeria, Godswill Akpabio kutoa zawadi ya gari mbili aina ya Toyota SUVs kwa mwanamuziki 2Face na mkewe Annie kimekuwa gumzo kwa watu mtaani hasa kutokana na gharama kubwa ya zawadi hizo.
Toyota Suv 'Prado' - Hii ndiyo model ya ndinga ambazo Mheshimiwa atawakabidhi maharusi
Gavana huyu katika kuonyesha kuwa hayo ni mambo madogo tu kwake, pia amesema kuwa halmashauri iliyo chini yake pia itagharamia usafiri kwa maafisa 29 ambao watahidhuria harusi rasmi ya msanii huyu ambayo imepangwa kufanyika huko Dubai tarehe 23 mwezi huu.
2Face na Annie
Kutokana na kitendo hicho, watu mbalimbali wamekuwa na mawazo tofauti hasa ukizingatia kuwa, gharama za vitu vyote hivi ni kutoka kodi za wananchi wa kawaida wa jimbo la Akwa Ibom Naijeria.

0 maoni:

Post a Comment

Labels