Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe akizungumza leo |
Tuzo za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, sambamba na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA kwa miaka mingine mitano.
Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Nembo Mpya |
George amesema Kilimanjaro Premium Lager imejizatiti kuendeleza
tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye
vipaji, lengo lao kubwa likiwa ni kuongezea thamani kazi na wasanii wa
hapa hapa nyumbani na pia kuwafungua macho watanzania kuzidi kuona
thamani ya muziki wa nyumbani pia kutambua mchango wa wanamuziki katika
kuleta maendeleo ya nchi.
Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania, dhamana ambayo sasa wanaishikilia kupitia tuzo hizi mpaka mwaka 2018.
Alikuwepo pia
Chidi Benz Chuma kuwakilisha wasanii wa muziki Tanzania ambapo
alizungumzia matarajio yake makubwa katika maboresho ya tuzo za mwaka
huu.
Some of the pictures courtesy of John Bukuku
|
0 maoni:
Post a Comment