Pages

Sunday, March 03, 2013

BAUCHA RECORDS KUTIMIZA MIAKA KUMI MWEZI HUU

Mwezi huu [Machi] 2013 Baucha Records Inatimiza miaka kumi sasa tangu kuanza kwake na Inampango wa kurudisha Talent Show itakayoanza Lindi na Mtwara mwezi Huu Then Mikoa ya Iringa na Mbeya mwezi Ujao yaani mwezi wa Aprili na mikoa mingine itafuata na washindi wataondokanao mpaka Dar es salaam kwaajili ya kufanyanao kazi na kazi hizo zitasambazwa Redioni.

Akipiga Stori kwanjia ya simu Leo asubuhi na Ergon Elly wa Kitulo Fm na Mmiliki wa Mtandao Huu Producer Mkongwe katika Industry Hii ya muziki wa kizazi kipya ALLY BAUCHA amesema katika pitapita huko wasanii kibao watapiga show akiwepo mwenyewe Baucha, K-One,Baghdad watapiga Show huko mikoani kwa Kijana mwenye kipaji jipange kwa wakati ndio huu wa kutoka kwao.

Na kama itawezekana Producer huyo na Msanii ambaye amenanya poa na Track yake ya Kelele aliyomshirikisha Ali Kiba atatambulisha ngoma katika Msimu huo wa kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Baucha Records

0 maoni:

Post a Comment

Labels