Pages

Thursday, March 28, 2013

MBUNGE AFARIKI DUNIA



MBUNGE wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), ambaye alidondoka jana ghafla katika mkutano wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amefariki dunia mchana wa leo hii.
MBUNGE wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), ambaye alidondoka jana ghafla katika mkutano wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amefariki dunia mchan huu.

 Salim alianguka jana saa tano asubuhi wakati akihudhuria mkutano wa kamati hiyo, uliokuwa ukifanyika katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam.
 Habari kutoka katika vyanzo vya kuaminika, zinasema licha ya madaktari kuonyesha jitihada za kuokoa maisha yake ya mbunge huyo, lakini harakati hizo zimegonga mwamba baada ya Salimu kupoteza maisha mchana leo hii.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wabunge wengine ambapo mkutano huo ulisitishwa kwa muda na juhudi za kumshughulikia zilianza, kwani alitolewa nje ya ukumbi na kuanza kupepewa.

Hata hivyo mbunge huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuingizwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alilazimika kutoka nje ya ukumbi ambapo aliungana na wenzake katika kuchanga mawazo kuhusu namna ya kumpeleka hospitali mbunge huyo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, hali ya mbunge huyo anayedaiwa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu iliendelea kubadilika, huku akitokwa na jasho jingi.

Kutokana na hali hiyo, mwishowe mbunge huyo alipoteza fahamu katika majengo ya Ofisi za Bunge, kitendo ambacho kiliwafanya wabunge wenzake kushindwa la kufanya.

Wabunge wanne walijaribu kumbeba mbunge huyo ili waweze kushuka naye chini, lakini walishindwa kutokana na uzito wake na hivyo wakalazimika kuomba msaada kwa waandishi wa habari.

Hata hivyo Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) aliwashangaza wenzake kutokana na kitendo chake cha kuwazuia waandishi wa habari kupiga picha kwa kuziba kamera zao akitumia makabrasha ya vitabu.

Waandishi wa habari watano walichukua takribani dakika nane kumbeba akiwa kwenye kiti hadi kumpeleka katika gari lenye namba za usajili STK 2178 Land Cruiser na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Nkamia alishangaza tena pale alipoacha kazi ya kusaidia kumbeba mwenzake, badala yake akaenda pembeni na kuanza kuvuta sigara, hali iliyofanya waandishi wabaki kumshangaa.

Akizungumzi tukio hilo, Lowassa hakuweza kueleza mazingira ya kunguka kwake, ingawa alithibitisha kwamba mbunge huyo aliugua ghafla na baadaye alianguka.

“Hivi sasa yupo ICU, kwani baada ya kumfikisha pale Muhimbili walimpeleka katika uangalizi maalum na timu ya madaktari inaendelea kumhudumia, taarifa za maendeleo ya afya yake tutaendelea kuzitoa,” alisema.
Mbali ya Nkamia, wabunge wengine waliokuwapo karibu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa Kikwajuni, Hamad Masauni na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF).

Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Salim Hemed Khamis (CUF) wa Chambani....Amen.

0 maoni:

Post a Comment

Labels