Pages

Friday, March 08, 2013

PICHA ZA CHRIS BROWN AKIWA NA WIZKID WAKIFANYA VITU ON STAGE


Ni mara chache sana kwa wasanii wakubwa wa muziki Marekani wanaotoa ushirikiano mzuri wakati wanapokuja Afrika kupafom, sio tu ushirikiano mzuri bali hata kujichanganya na wasanii wa Afrika wanaokuwepo kupafom nae kwenye stage moja.
Time hii zali limemdondokea staa Wizkid wa Nigeria ambae kwa mara ya pili mfululizo mwimbaji staa Chris Brown amemuita kwenye stage na kupafom pamoja huko Ghana juzi ambapo kwa mara ya kwanza alimuita wakati akipafom kwenye mji wa Lagos Nigeria.
Uhusiano wa wawili hawa unazidi kukua na unatoa nafasi ya wengi kuamini kwamba kolabo au ushirikiano mkubwa zaidikwenye kazi za wawili hawa vinaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa.
Ni stori ambayo imechukua headlines sana kwa sababu wasanii wengi wa Marekani wanapokuja Afrika wengine hukataa hata kupiga picha au kukaa sehemu moja backstage na wasanii wa Afrika, wengine pia hawaruhusu kabisa Video Camera iwachukue wakipiga picha na watu manake wanaogopa inaweza kutumika kibiashara.

0 maoni:

Post a Comment

Labels