Louise na Martine Fokkens wakiwa kazini.
MAPACHA wenye umri wa miaka 70 nchini Amsterdam, Uholanzi, wameamua
kustaafu kazi yao ya ukahaba baada ya kuifanya kwa miaka 50. Mapacha hao
Louise na Martine Fokkens wameamua kustaafu baada ya umri kuwatupa
mkono na kudai kuwa kwa sasa hawapati wateja.
Louise na Martine wamelala
na jumla ya wanaume takribani 355,000, kila mmoja akiwa amejivinjari na
wastani wa wanaume 177,500 kwa kipindi cha miaka 50, ambapo kwa mwaka
mmoja kila mmoja alikuwa analala na wanaume 3,550 sawa na wanaume 295
kwa mwezi na kwa siku wanaume 9.
Mapacha
hao ambao wanadaiwa kuwa makahaba wenye umri mkubwa zaidi jijini
Amsterdam, walianza kazi hiyo wakiwa na umri wa miaka 20. Mapacha hao ni
wazazi wa watoto saba, Louise akiwa na watoto wanne, na Martine yeye
ana watoto watatu.
Mapacha hao ambao walikuwa wakipenda kuvaa sare ya
nguo nyekundu walitoa Filamu ya simulizi za kweli iitwayo 'Meet the
Fokkens' na wanatarajia kutoa kitabu kitakachoelezea safari yao katika
biashara ya ngono.
0 maoni:
Post a Comment