Mabingwa
watetezi, Simba wamefufuka katika jinamizi la matokeo mabovu baada ya
kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Wagosi Coast Union.
Simba ambao
walianzisha wachezaji wengi wa kikosi cha vijana walionekana kuwa na
uchu wa mabao toka dakika ya mwanzo huku Mrisho Ngassa akionekana kuwa
mwiba mkali kwa walinzi wa Coastal Union, na ilikuwa ni katika dakika ya
45 alipoipatia bao la kwanza.
Wakati bado Coastal wakitafakari nini
kimetokea, Haruna Chanongo alifunga bao la pili baada ya kugongeana
vizuri na Ngassa na hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza.
Kipindi
cha pili Coastal walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Razack
Halfan huku Simba wakiendelea kumiliki mpira kwa asilimia kubwa. Hadi
mwisho Simba 2-1 Coastal Union.
0 maoni:
Post a Comment