Akiongea na gazeti la Mwananchi, Hemedy alisema mkataba huo
utamfanya yeye kufikiria zaidi filamu zake kuliko kucheza kwenye filamu
za watu wengine.
Aliliambia gazeti hilo kuwa ubize huo wa mwaka pia ndo unamfanya
kushindwa kuanza kutengeneza nguo za ndani za wanawake kama alivyosema
mwaka huu kuwa anatarajia kuanza kubuni nguo zake za kike za ndani za
wanawake.
“Watu kila siku wanajitokeza wanabuni tisheti, makoti na vitu
vingine, mimi nilikaa chini nikafikiria kwanini mama zetu, dada zetu
wanaenda kununua nguo za ndani za mtumba Mwenge na kwenye masoko
mengine? Nikaona si kitu kizuri kwa kuwa hizo zimetoka nje ya nchi na
zimeshavaliwa kwa hiyo mimi ndo nikaona nibuni nguo za ndani kwa ajili
yao,”aliliambia gazeti hilo la kila siku.
Pia alidai kuwa ana mpango wa kurudi shule kumalizia ‘Degree’ yake ya
Masoko ambayo alishaanza lakini alishindwa kuendelea kutokana na kazi.
0 maoni:
Post a Comment