Pages

Saturday, March 09, 2013

MAELEZO YA RAMA D KUHUSU WIZI WA KAZI YAKE - TIGO

Kupitia mtandao wa kijamii pendwa Facebook Msanii Rama D ambae anafanya vizuri na nyimbo yake ya "KUWA NA SUBIRA" ametoa maelezo yake kuhusu issue ya nyimbo yake kutumika kwenye caller tune bila ruhusa yake wala mkataba wowote.

Rama D amefunguka kwa style hii

"Napenda kuwapa taharifa Mashabiki wangu Wapenzi wa Muziki wangu na Ndugu Zangu wenye mapenzi Na Muziki wangu kuwa naskitika na naskia uchungu Sana Kwa kampuni ya sim Tigo kwa kuuza Kazi yangu ya "Kuwa Na Subira"toka mwaka jana mwezi wa 6 Bila makubaliano na Muhusika mkuu ambaye ni Mimi Rama Dee tafadhari ndugu zangu naomba mnisaidie sitaki kupita njia nyingine zaidi ya hii kuweka ukweli hapa..
 
naumia sana sana kuona Tigo inanikandamiza inafananya biashara Ambayo sio halali,najuwa ndani ya Wapenzi wa Muziki wangu kuna Wansheria na Waandishi wa Habari pia wapo watu wenye Blogs na Web naomba mnisaidie kuwajulisha wananchi juu ya Manyanyaso ya Kampuni hii ya simu Tigo Hii inaonyesha ni jinsi Gani hakuna haki wala heshima kwenye sanaa,pia kutumia njia ambayo haitambuliki kuwadanganya Wananchi kuwa hiyo ni kazi halali ambayo imetoka kwangu..
 
Ndugu zangu Tigo wanaharibu Mahusiano yangu na Nyie Mashabiki wangu Kwa maana wanauza kazi kwa njia sio halali...Kama umenunuwa Kazi yangu Ya Kuwa Na subira Tigo basi juwa wamekudhurumu haki yako ambayo ilikusudia kunichangia mimi."
 
Habari Kwa Hisani http://hassbaby.blogspot.com

0 maoni:

Post a Comment

Labels