Pages

Friday, March 08, 2013

UJUMBE KUTOKA KWA MSANII DAYNA KUHUSU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.


Dayna
Naitwa Dayna Nyange. Mwanamuziki wa Bongo Freva. Ni Mwanamke wa KiTanzania. naungana na wanawake wengne duniani kote katika kuadhimisha Siku ya wanawake duniani.  Nawashauri wanawake wenzangu juu ya kujituma kufanya kaz ili kujipatia maendeleo bila kutegemea wanaume. 
 
Naamini  wenyewe tunaweza  tena bila ata ya kuwezeshwa.  Nakupitia siku hii muhimu kwetu naiomba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha inapambana vilivyo juu ya unyanyasaji wa kijinsia  tunaoupata wanawake. 
 
hasa ubakaji, ukeketaji na  mauaji yanayoendelea zidi  yetu, tunaiomba serikali ihakikishe kwamba wahusika wa matukio kama hayo wanachukuliwa hatua za haraka ili kukomesha maovu hayo. 
 
Pia nijukumu la kila mwanamke na  Niwajibu wetu kina Mama pia na jamii kwa jumla kupambana na majanga haya. tushikamane kujiletea. Tupendandane tushikamane WANAWAKE TUNAWEZA By Dayna Nyange.

0 maoni:

Post a Comment

Labels