Pages

Sunday, August 18, 2013

ASIMULIA ALIVYOTUMIA POLISI KUMPATA MKE WAKE...

 Zahir Zoro (Kulia) akiwa na mtoto wake Banana Zoro 
Na Kalunde Jamal, Mwananchi 
“Kipindi hicho tukiwa Mafinga rafiki yangu mkubwa alikuwa ni Emmanuel Mpangala ambaye alikuwa akifanya kazi RTC, sasa nilipokuwa nakwenda kumtembelea ndiyo nikamwona binti mrembo wa kutoka kandokando ya Ziwa Nyasa Angela Mahinya ambaye kwa sasa ni marehemu,” anaanza kusimulia Zahir kwa masikitiko yaliyochanganyika na huba.

Dar es Salaam. Zoro anasema kuwa mwaka 1981 walihamia Mafinga na ndiyo chimbuko hasa la kumpata mkewe huyo ambaye anasimulia kuwa uhusiano wao ulikuwa wa kihistoria.
“Kipindi hicho tukiwa Mafinga rafiki yangu mkubwa alikuwa ni Emmanuel Mpangala ambaye alikuwa akifanya kazi RTC, sasa nilipokuwa nakwenda kumtembelea ndiyo nikamwona binti mrembo wa kutoka kandokando ya Ziwa Nyasa Angela Mahinya ambaye kwa sasa ni marehemu,” anaanza kusimulia Zahir kwa masikitiko yaliyochanganyika na huba.
Anasema akiwa anakwenda hapo mara kwa mara wafanyakazi wengi walikuwa na shauku ya kumwona na kuongea naye kwa kuwa alikuwa ni mwanamuziki anayefahamika, hivyo siku moja Mpangala akamwambia kuwa Angela anataka kumwona, wakati huo alikuwa hamfahamu zaidi ya kumwona juu juu akiwa katika kazi zake.

Anaendelea kueleza kuwa cha kushangaza siku walipokutana na kuongea akiwa ofisini kwake alipoteza ujasiri wa kiume aliokuwa nao, kwani aliona anasisimka hadi nywele na kuona kuwa huyu anaweza kuwa ni mwanamke anayestahili kuwa mpenzi wake.

“Nilipoteza ujasiri mbele ya Angela kwa mara ya kwanza tu nilipomwona na kujikuta akiniuliza jambo badala ya kujibu nabaki namwangalia, nikajikaza na kurudi katika hali ya kawaida ingawa bado mara nyingi nilikuwa sielewi,” anasema Zoro.

Anafafanua kuwa baada ya kukaa kwa muda ofisini kwake wakapanga siku ambayo walitoka wote kwenda sehemu kuzungumza na kuanzia hapo akawa anakwenda nyumbani kwake kama rafiki, huku akiogopa kumwambia hisia zake akiamini anaweza kuvunja hata urafiki wao.

Anasimulia kuwa ilimchukua muda kumwingiza katika 18 zake licha ya kupewa msaada na Mpangala.

Zoro anasema baadaye Angela aligeuka kuwa mpenzi wake bila kujua kutokana na kuwa na mazoea ya kuwa pamoja kila wakati ikiwamo kwenda muziki pamoja usiku.

Anaendelea kusimulia kuwa wakiwa katika uhusiano siku moja akaambiwa na Angela kitu kilichomshtua kuwa mtu mmoja amewaambia kuwa yeye ana mke jijini Dar es Salaam ambaye ni Brigedia wa Jeshi hivyo wakati wowote ataingia matatani.

Angela alianza kuomuogopa hali iliyomfanya wasikutane tena mara kwa mara.

”Hali ilikuwa mbaya upande wangu, mwanamke unayempenda na uliyemsotea kwa muda mrefu anakuja mtu anamwambia maneno ambayo yanatishia uhusiano wenu we acha tu”

Zoro anasema ili kumthibitishia kuwa hakuwa na mke alichukua Angela akasafiri naye hadi kwa mama yake jijini Dar es Salaam ili athibitishiwe kuwa yeye hakuwa na mke. Anasema alimueleza mama yake uamuzi wake wa kuoa Angela na mama yake akakubali.

0 maoni:

Post a Comment

Labels