Pages

Wednesday, August 21, 2013

MSANII MAVADO AGOMA KUSAFIRI KWA NDEGE TOFAUTI NA ALIYO AHIDIWA NA WAANDAJI WA SHOW HUKO JAMAICA

Mavado Msanii mkali wa miondoko ya Dancehall kutoka huko Jamaica, amekuwa gumzo hasa baada ya kukataa kwenda kufanya show huko Guyana baada ya waandaaji wa show hiyo kumtumia usafiri wa kandege kadogo badala ya Jet ambayo walimuahidi.

Msanii huyu na timu yake ya watu 17, waliipotezea show hii kubwa na kurudisha hasara yote kwa muandaaji ambaye mpaka sasa hajasema chochote katika vyombo vya habari kuhusiana na tukio hili.

Jitihada pia zinaendelea kumtafuta msanii huyu ama uongozi wake kufahamu zaidi mustakabali wa tukio hili na issue nzima ya kulipana fidia kama itakuwepo.

0 maoni:

Post a Comment

Labels