Pages

Friday, August 16, 2013

MRISHO NGASSA AIDHINISHWA KUICHEZEA YANGA - KWA SHARTI LA KUILIPA SIMBA MILLIONI 45


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga
baada ya kukamilisha usajili wake.
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi
ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha
fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50
(sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.SOMA ZIDI BOFYA HAPA
Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya
Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi
hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi
atakapolipa fedha hizo.Na Shaffih dauda
Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu
usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka
klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi
(Agosti 22 mwaka huu).
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe
kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili
kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi
Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo
hazikuafikiana.

0 maoni:

Post a Comment

Labels