Pages

Tuesday, August 20, 2013

HALI YA KIAFYA YA MEMBER WA B2K ''RAZ B YAENDELEA VIZURI HII NI MARA BAADA YA KUPIGWA NA CHUPA KICHWANI



 Alhamisi ya wiki iliyopita (August 15), aliekuwa mwimbaji wa kundi la B2K Raz-B, alijikuta katika chumba cha watu mahututi baada ya kupigwa na chupa kichwani katika moja ya show alizokuwa akifanya nchini China.
Raz-b (28) alikuwa akifanya show kwenye moja ya kumbi za starehe Zhejiang, China wakati ugomvi ulipotokea upande wa mashabiki wameripoti TMZ.
 
Inasemekana Raz alienda kusuluhisha huo ugomvi wakati jamaa mmoja alipo vurumusha chupa iliyompata kichwani na kupelekea kukatwa sehem mbali mbali na kumchana sana kwenye mdomo wake na kusababisha kufanyiwa operation ya saa  moja kurekebisha shimo kwenye mdomo wake  iliyokuwa pia ikihitaji nyuzi 4.

siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji hali haikuwa nzuri, hakuweza kuamka na mmoja wa ma dancers wake alimkimbiza hospitali ya karibu na hali yake kusemekana kuwa mbaya kiasi cha kufikia kupumulia mashine.
Raz-b amekua akiishi China kwa miaka 3 sasa na ana plan za kurudi marekani 
UPDATE: Hali ya Raz kwa sasa inaendelea vizuri, anapumua mwenyewe bila kutumia mashine na anaongea na kucheka la bado hajaruhusiwa kutoka hoospitali.. amesema mmoja wa watu wake wa karibu.
muwakilishi wa Raz amesema "Doc amesema ni maajabu ame-survive"

0 maoni:

Post a Comment

Labels