Wakati unaingia nyumbani kwa bilionea Erasto Msuya hili ndio bango lililokua limewekwa.
Hii ndio nyumba ya milele ya bilionea Erasto Msuya ikiandaliwa.
MIRERANI
zikiwa ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya
Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi zaidi
ya ishirini na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe
karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport). Kifo
hicho kilichokua na utata mkubwa na kupelekea watu wengi kujiuliza
maswali mengi yasiokua na majibu. Leo ilikua ni siku ya mazishi ya
mfanyabiashara huyo ambaye kutokana na kuwa alikua akiishi jijini Arusha
maeneo ya kwa Iddi ilibidi jana jumatatu wafanye utaratibu wa kuuga
mwili wa marehemu nyumbani kwake na leo jumanne kwenda kuzikwa Mirerani
katika kijiji cha Kairo.
Msiba wa Erasto ulikua ni gumzo kubwa sana na watu wamekiri hawajawai
kuona msiba kama huu maana kilichokua kikiwashangaza watu ni jeneza
lililokua likifunguliwa kwa rimoti, na pia ni mazishi yaliyokua na watu
wengi sana. Kila kona kulikua na minong'ono ambayo ilikuwa ikizungumzia
utata wa kifo chake. Kamati ya maandalizi ya mazishi wakishirikiana na
ndugu, jamaa na marafiki walijitahidi sana kuhakikisha kila kitu
kinakwenda sawa maana haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu kuhakikisha
usalama wa wingi wa watu uliokuwepo katika mazishi ya Erasto.
Kwa picha za matukio zaidi kuhusiana na mazishi ya bilionea Erasto endelea kutembelea www.kingjofa.blogspot.com
0 maoni:
Post a Comment