Msanii wa muziki wa
kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa
Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Sehemu ya umati wa watu
waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku wa kuamkia leo
wakiburudika na wasanii wa Serengeti Fiesta 2013.
Burudani ya kutosha kabisa.
Palikuwa hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi, Christian Bella akikamua jukwaani.
Msaniii anekuja kwa kasi
kwenye miondoko ya Hip Hop, Stamina akikamua jukwaani usiku wa kuamkia
leo mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye
tamasha la Serengeti Fiesta.
Ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Yaani hapatoshi kabisa, wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT, akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani.
Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini burudani hizo.
Wadau nao walitokelezea.
Peter Msechu na madansa wake wakikamua vilivyo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Pichani ni msanii wa
Bongofleva, Shilole Mohamed na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi
wa Kigoma, waliojitokeza kwa wingiusiku wa kuamkia leo kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
0 maoni:
Post a Comment