Pages

Wednesday, August 21, 2013

PRODUCER SCOT STORCH AIBIWA NA WAHUNI



Scot Storch Producer mkali wa muziki ambaye amekuwa ni mtu wa matukio sana  amekumbwa na maswahiba makubwa hasa baada ya kubananishwa na wahuni na kuibiwa pesa pamoja na vito vya dhahabu vyote alivyokuwa amevaa wakati alipokuwa akitoka katika hoteli ya New York Palace Madison Avenue.

Producer huyu amedai kuwa alifuatwa akiwa katika gari na watu waliokuwa na bunduki na kumuamrisha atoe kila alichonacho ama wangemwua,na producer huyu hakuwa na pingamizi zaidi ya kuwakabidhi briefcase iliyokuwa na dola zipatazo 5000 cash pamoja na vito alivyokuwa amevaa vyenye thamani inayofikia dola 100000, na jumla ya vitu alivyopigwa staa huyu vinafikia thamani ya shilingi 169,522,500/- za kitanzania.

Kwa sasa polisi wanaendelea kufuatilia issue hii baada ya kupata taarifa rasmi kutoka kwa Scot mwenyewe ambapo pia kwa sasa anakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kushindwa kusimamia jukumu la kumlea mtoto wake inavyotakiwa.


0 maoni:

Post a Comment

Labels