Pages

Monday, October 28, 2013

Chris Brown Akamatwa Na Polisi Washington DC

Mwanamuziki wa Pop na R&B Chris Brown akamatwa leo saa  4:25 a.m. asubuhi (0825 GMT) na kutiwa mbaroni na Polisi akiwa jijini Washington DC Marekani kwa kosa la kupigana na mtu ambaye haikujulikana ana uhusiano gani na msanii huyo, mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Christopher Hollosy na yeye pia alikamatwa na polisi lakini alipelekwa Hospital kwanza.


chris_brown_lead_1
Chris Brown ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kazi za kusaidia jamii kutokana na kosa la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna na pia hivi karibuni kukutwa na hatia ya kugonga mtu na kukimbia jijini Los Angeles ambapo aliongezewa adhabu ya kusaidia kazi za kijamii kwa muda wa masaa 1000.

Ofisi ya uwanasheria jijini Los Angeles imemshtaki mwanamuziki huyo kwa kosa la kukwepa kutumikia adhabu yake ambayo Chris Brown anatakiwa kuitumikia baada ya kupewa ruhusa ya kutumikia adhabu hio nyumbani kwao Virginia.

0 maoni:

Post a Comment

Labels