Pages

Monday, October 21, 2013

HIZI NDIZO SABABU ZA MR BLUE ZA KUTOONEKANA KWENYE VIDEO YA HEMEDY PHD - REST OF MY LIFE

 
Blue amesema "Ni kweli Hemedy alinitafuta tufanye video ila wakati huo nilikuwa na show nje ya nchi na nilivyo rudi sikuwa na nafasi ila tulikubaliana kuwa tuta shoot hivi karibuni, Blue amendelea kusema  Ameshanga sana kusikia kuwa video imetoka bila yeye kuwepo na kuwa Hemedy amechana mistari yake, Sina sababu ya kutokuwepo kwenye video ya Hemedy kwani sisi ni marafiki na nampa heshima sana Hemedy kama kaka yangu, Nikimuona Hemedy nitamuliza kwanini ameshindwa kusubiri mpaka niwe na muda wa kufanya sehemu yangu na ametoa video bila mimi"
Mr Blue Alimaliza kwa kusema kuwa Atakacho fanya ni kumtafuta na wayamalize na kama kutakuwa na version ya pili ya hii video basi anauhakika wa kuwepo kwenye kipande chake alisema

KWA UPANDE WA HEMEDY PHD
 
HEMEDY PHD AWAOMBA LADHI FANS WAKE KWA KUTOONEKA MR BLUE KWENYE VIDEO YA WIMBO WA REST OF MY LIFE.
The Hit Maker wa Track ya Rest Of My Life nazingine Kibao ''Hemedy PHD'' Aliyomshirikisha Mr Blue Amewaomba Ladhi Mashabiki wake kwa Kutooneka Mr Blue kwenye Video ya Wimbo Huo ambayo imeachiwa Rasmi Leo.

Hemedy amesema kuwa Kutokana na Mr Blue Kuwa na Tour nyingi nje ya Nchi ndiyo sababu kubwa iliyofanya Mr Blue kutoonekana kwenye Video hiyo hii nikutokana na yeye Kutaka kuwahi kuitoa Video Hiyo.


PHD Ameongeza Kuwa Licha ya Video hiyo kutoka lakini atafanya Version ya Pili ambayo itamuhusisha Mr Blue na inatarajiwa kuanza kufanyika mapema kabla ya Mwaka Huu Kuisha itakuwa Tayari imetoka.

Akipiga Stori katika Kipindi Cha BEST REQUEST...online www.bestfm.co.tz kinachorushwa na BEST FM ya Mkoani Njombe wilaya ya Ludewa amesema anampango wa Kurelease New Joint nyingine ambayo amemshirikisha Bi - Dadakuwa na Mapema Mwazoni mwa Mwaka 2014 ataachia Filamu yake ambayo kwasasa Inafanyiwa uhariri/Editing.


0 maoni:

Post a Comment

Labels