Wamiliki
wa supermarket ya Village Market ya nchini Kenya wamejitokeza na kudai
kuwa vitu vilivyokuwa kwenye kontena lilikamatwa Mombasa ni vya kwao.
Wamesema waliagiza vitu hivyo kutoka China kwaajili ya sikukuu ya Kimarekani ya Halloween baadaye mwezi huu.
Katika maelezo yake, wameandika:
Market Masters LTD, hereby confirms
that indeed we have ordered for the Halloween decorative items imported
from China in container number PCIU 8125750, and are not restricted
items.
Just like during Easter Holiday or
Christmas season, the items in question are solely used for decorating
the entire shopping centre for our annual Halloween parties held within
village market every last Saturday in October, for the past 17 years.
We needed to replace the old worn out ones with us, in readiness for our upcoming Haloween party slated for 26th October 2013.”
Kontena hilo lilikuwa na wanasesele
wa kutisha, wanaonekana wakiwa na maumivu makali, mikono na miguu
iliyokatwa, maiti na vitu vingine vilivyodaiwa kuwa vya kishetani.
Awali, vitu hivyo vilidaiwa kuwa vya
mwanasiasa maarufu wa Kenya, aliyewahi kuwa naibu waziri wa zamani,
Omingo Magara ambaye alilazimika kujitokeza na kukanusha japo alikiri
kuwa baadhi ya vitu vyake (tofauti kabisa na vitu hivyo vya ajabu)
vilikuwemo ndani ya kontena hilo.
Na sasa ameitaka mamlaka ya mapato nchini humo, KRA kumwomba radhi na kama ikishindwa ndani ya siku 7 ataipeleka mahakamani
0 maoni:
Post a Comment