Pages

Wednesday, October 09, 2013

MSANII NONINI WA KENYA AELEZA SABABU YA KUACHA KUTANGAZA REDIO,NA PIA KUHUSU UWEZEKANO WA YEYE SIKU MOJA KUINGIA KWENYE SIASA.


Nonini kipindi hicho akitangaza kipindi cha asubuhi Katika kituo cha One Fm huko nchini Kenya.


Msanii Nonini Mgenge kutoka Nchini Kenya ambaye pia alikuwa mtangazaji wa kituo cha One Fm amesema kuwa ameacha kazi hiyo ya utangaji kutokana na sababu zake binafsi ambazo hayuko tayari kuziongelea.
Nonini alisema pamoja na hayo utangazaji ni kazi anayoanaipenda na hawezi kuiacha kabisa hivyo ataendelea kuifanya.

Msanii huyo alisema kuwa wakati anafanya kazi hiyo alikuwa anapata wakati mgumu kupiga nyimbo zake lakini ilimbidi wakati mwingine apige pale unapokuta wasikilizaji wengi wameuomba.
Msanii huyo ambaye aliwahi kutajwa na mtandao mmoja kama msanii wa muziki mwenye likes nyingi zaidi kuliko wasanii wote Africa ya Mashariki alisema pamoja na ushawishi wake kwenye mitandao yake,na brandy ya jina lake hana mpango wowote wa kuja kuingia kwenye siasa.

0 maoni:

Post a Comment

Labels