Pages

Saturday, October 19, 2013

Nicki Minaj asema Queen Latifah ndiye aliyewafungulia njia Rappers wa kike!!

Video: Nicki Minaj asema Queen Latifah ndiye aliyewafungulia njia rappers wa kike
Nicki Minaj ameutambua mchango wa rapper mkongwe Queen Latifah, kwa kudai kuwa ndiye aliyewafungulia milango mcees wa kike akiwemo yeye mwenyewe.

Nicki Minaj alisema hayo kwenye kipande cha mahojiano aliyoyafanya kwenye 'The Queen Latifah Show' yatakayorushwa October 22.

“Umefungua milango mingi kwangu na kwa wanawake wengine na siku zote huwa nakutaja wewe ninapoongelea rappers wa kike waliyoitengeneza njia ya mwanamke mfanyabiashara na nguli katika kila kona ya burudani,” alisema Nicki Minaj.

“Kukaa hapa kufanya kipindi chako, ni wasaa muhimu wa Hip Hop. Hivyo, asante kwa kunileta hapa.”

0 maoni:

Post a Comment

Labels