Pages

Sunday, October 06, 2013

KAMETA PRODUZA ALIYEMTOA MSANII HUYO KIPINDI HICHO ASEMA "NAMTAFUTA MR NICE",

Produza Kameta akiwa kwenye studio yake TIKA Production

Produza Kameta ambaye alifanya kazi na Mr Nice kipindi ambacho msanii huyo anaanza muziki amesema kuwa msanii huyo anahitaji msaada hivi sasa na si wakati wa kumlaumu.Produza huyo ambaye alifanya album ya kwanza ya Mr Nice 'Kidalipo' iliyokuwa na nyimbo kama 'Kikulacho', 'Kidalipo' na nyingine ambazo ndo nyimbo zilizomtambulisha msanii huyo kipindi hichi kwenye ramani ya muziki Tanzania.
Mr Nice alipata nafasi ya kupata mkataba katika studio za GrandPa Rec zilizoko nchini Kenya lakini mkataba wake ulisitishwa baada ya GrandPa kutangaza kuwa msanii huyo ni msumbufu na hafanyi kazi kwa muda kutokana na kunywa pombe nakusahau muda wa kazi.Baadae msanii huyo alichukuliwa na lebo nyingine ya huko Kenya Candy n Candy lakini hivi sasa inasemekana msanii huyo yuko Tanzania baada ya kushindwa kufanya kazi na lebo hiyo.
Produza huyo alisema yeye binafsi amefanya juhudi za kumtafuta msanii huyo kwa njia ya simu lakini namba aliyonayo haipatikani mpaka leo

0 maoni:

Post a Comment

Labels