Pages

Wednesday, October 09, 2013

JAY MOE AWAKUTANISHA WASANII ''MR BLUE,CPWAA NA A.Y KATIKA STUDIO ZA BONGO RECORD'S (CBM)

Jay Moe awakutanisha Mr. Blue, Cpwaa na AY ndani ya Bongo Records (CBM), Mr.Blue aielezea
Mteule Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe, More Techniques amewakutanisha wakali wa Bongo Fleva Mr. Blue, Cpwaa na AY kwa kuwashirikisha kwenye wimbo wake unaotarajiwa kutoka hivi karibuni na umepikwa na producer P-Funk Majani wa Bongo Records.

Wimbo huo umepewa jina la CBM ikimaanisha ‘Check Bob Maarifa’. Mmoja kati ya washiriki katika Project hiyo Mr.Blue Byser ameongea na tovuti ya Timesfm kuhusu project hiyo ambapo amesema project hiyo ni kubwa na iko chini usimamizi mkubwa.

“Mi naweza kusema Project ni nzuri, na ni project kubwa, kama unavyoona imefanywa na watu hawa wakubwa.
 
Pia ni Project ambayo ina nguvu sana, kwa hiyo usimamizi wake ni mkubwa chini ya P-Funk Majani mwenyewe au sio..
 
kwa hiyo fans wa Jay Moe wategemee kitu kikubwa sana kutoka kwa Jay Moe, na fans wa CP hali kadhalika fans wa AY na Mr. Blue.” Amesema Byser.

P Funk Majani ametweet kuhusu ngoma hiyo ya Jay Moe ambae yuko nje ya nchi hivi sasa, BMS inaweza kusikika kwenye vituo vya radio hivi punde kwa mujibu wa Majani. 
 
So endelea kusikiliza Timesfm 100.5 au kama uko nje ya Dar es Salaam unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii. 
 
“CBM Coming Soon to a Radio Near You!” Ametweet P-Funk Majani.

0 maoni:

Post a Comment

Labels