Mshambuliaji
nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema kuwa hasira zake ni kama
atashindwa kufunga au angalau kutoa pasi itakayozaa bao litakaloimaliza
Simba:
“Niko vizuri na ninajiona niko tayari kwa mchezaji, nataka kufanya kazi nzuri na ninajua Simba nitawafunga. Kama nitashindwa kufunga basi nitatoa angalau pasi ya bao litakalosababisha Simba wafungwe. La sivyo nitachoma nyumba zangu tano ninazomiliki,” alisema Ngassa kwa kujiamini.
Yanga na Simba zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment