Pages

Wednesday, October 16, 2013

Snoop Liom abadili tena jina lake, sasa anaitwa SnoopZilla


Snoop Dogg kama anavyofahamika kwa wengi alianza kubadili jina lake kuwa Snoop Lion kwa madai kuwa amezaliwa upya na ameingiliwa na mzimu wa marehemu Bob Marley na kuamua kufanya album ya reggae kwa jina jipya ‘Snoop Lion’, ametumia sababu kama hizo tena kubadili jina hilo tena.
Snoop ambae anafanya Project ya kumuenzi mwimbaji mkongwe na  funk bassist, Bootsy Collins maarufu kama Bootzilla, amesema ameamua kubadili jina lake na kuwa SnoopZilla ili kuendana na kile anachokifanya sasa.
Snoop sasa ameunda band mpya aliyoipa jina la 7 Funk Days akiwa na Dam Funk, na wameshatengeneza album wakiwa kama 7 Days of Funk.
7 Days of Funk wataachia album yao December 10, tayari Dam Funk na SnoopZilla wameachia wimbo wenye ujumbe wa mapenzi ‘Faden Away’.

0 maoni:

Post a Comment

Labels