Pages

Wednesday, October 09, 2013

KABLA MWAKA 2013 HAUJAISHA LINEX ATADONDOKA NA HUU MCHONGO SIKILIZA


Msanii anayefanya vizuri na wimbo wa 'Kimugina' Si mwingine ni Linex The Voice Of Africa amesema kuwa kabla ya mwaka haujaisha amepanga kuachia wimbo ambao utawahusu waliolewa na hata ambao hawajaolewa.'Unataka Ndoa au Unataka Harusi ndo jina la wimbo huo.



Linex alieleza sababu yakutaka kutoa wimbo mwingine wakati bado wimbo wa 'Kimugina' unaendelea kufanya vizuri na pia huo utakuwa ni wimbo wake 3 kwa mwaka huu.”Mimi naandika sana, hivyo nina nyimbo nyingi kwahiyo sioni sababu ya kukaa na nyimbo”, Linex.


Alisema kuwa beat ya wimbo imetengenezwa na Fundi Samweli,halfu vocal anatarajia kufanya na Tudd Thomas.Wakati huo huo alisema tayari ana video ya wimbo wa 'Kimugina' na muda wowote mashabiki wake wataanza kuona wimbo huo kwenye TV.

0 maoni:

Post a Comment

Labels