Pages

Monday, October 21, 2013

SIMBA WAONGOZA DHIDI YA YANGA KATIKA ''NANI MTANI JEMBE''?

Pamoja na mchezo wa watani wa jadi kuisha kwa sare ya 3-3 Jumapili ya wiki iliyopita, Simba wameanza kuongoza katika kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inayoendelea hivi sasa kwa kuwashirikisha mashabiki wa klabu hizi mbili kongwe nchini.


Mpaka sasa Simba wana kitita cha Shilingi 50,012,500.00 wakati watani wao wa jadi Yanga wana Shilingi 49,987,500.00. 

Upigaji wa kura katika kampeni hii unahusisha mashabiki kununua Bia ya Kilimanjaro na kusoma namba zilizo chini ya kizibo na kutuma kwa ujumbe wa simu wakianza na jina la timu wanayoishabikia kwenda 15440 na moja kwa moja Shilingi 1,000 kupunguzwa kutoka kwa wapinzani na kuwekwa kwa timu yao. 

Matokeo ya Nani Mtani Jembe yanapatikana katika tovuti ya http://kilitime.co.tz/campaigns/nmj/

0 maoni:

Post a Comment

Labels