Pages

Thursday, November 22, 2012

BRAND NEW MUSIC;-LADY ZHENA - NILITELEZA




NAMTAMBULISHA LADY ZHENA…..AWAPA SOMO WANAMUZIKI WA KIKE!!

Wapo wanamuziki wa chache wa kike wanaopiga muziki wa kizazi kipya, kwa sasa, lakini kadri siku sinavyokwenda, wanaendelea kuibuka wanamuziki kadhaa wa kike ambao kwa hakika wanajitahidi kuziteka nyoyo za wapenzi wa muziki wa kikazi Kipya.

Mmoja wa wanamuziki hao ambaye ameamua kufunguka na kueleza ya moyoni mara baada ya kuingia rasmi katika tasnia hii ya muziki wa kizazi kipya ni mwanamuziki Lady Zhena.

Lady Zhena anaeleza kinagaubaga kuwa ni vyema wanamuziki wa kike nchini kutambua kuwa, wanapaswa kuwa na moyo wa uvumilivu na kutokata tamaa mapema kwani hakuna maendeleo ya ghafla na ya haraka.

Anasema wanamuziki wa kike wanapaswa kutilia maanani mazoezi na kujifunza mbinu za muziki zitakazowawezesha kutunga na kuimba kwa sauti tamu kama wanavyofanya wenzao wanaong’ara hapa Afrika.

Anasema Inafaa pia kwa wanamuziki wetu wa kike kuithamini kazi hiyo kwa kuiona kuwa sawa na zingine, tena isiyopaswa kuchezewa.

Isiwe tu wanapotoka stejini, basi wanajiona na kazi ndio imekwisha.

Ni vyema pia kwa wanamuziki wa kike kujiheshimu wakati wote.

Iwapo watajiheshimu wawapo kwenye muziki, ni rahisi pia kwao kuheshimika kwa mashabiki.

Lady Zhena amefunguka na kusema kuwa  maendeleo ya wanamuziki wa kike na kung’ara kwao kimuziki, kutaamsha hamasa kwa wanawake wengi wenye vipaji kujitokeza, badala ya ilivyo hivi sasa, ambapo wengi wanasita kwa kuiona fani hiyo ni ya kihuni.

Mwisho Lady Zhena, anaomba Support kwa watanzania waipokee kazi yake mpya na kuomba baraka za Watanzania, kwani bila wao yeye si mali kitu.

Single yake mpya aliyoitoa hivi karibuni katika Audio na Video, aliyomshiriisha B- Baros imeanza kufanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari, ikijulikana “Niliteleza” chini ya Usimamizi wa Brabe Entertainment.

 ENDELEA KUTEMBELEA MTANDAO HUU ILIKUDOWNLOAD WIMBO HUO

0 maoni:

Post a Comment

Labels