Pages

Friday, November 23, 2012

50 CENT NA BOSS WA YMCMB WAWEKA BEEF PEMBENI

 

Ni kama ndoto vile mtu mzima 50 Cent na Birdman wameweka beef pembeni na kutoa kama shukurani kwa waturuki.

Marapper hawa wenye majina makubwa kwenye HipHop duniani wamechukuwa time yao kutoa ahsante yao kwa kuwalisha watu wa jamii zao.

Fifty akiwa ameungana na ‘Feeding America’, the Food Neywork na SMS Audio amekula chakula cha pamoja na wahanga wa kimbunga cha sandy kwenye event iliyopewa jina la “Our Table Is Yours” ambayo ilisimamiwa na Cipriani Restaurant huko Manhattan.


Wakati Fifty akifanya hayo Birdman yeye ameungana na mwana hisa mwenzake ambaye ni kaka Ronald “Slim” Williams na kutoa turkeys 2000 kwa familia mbalimbali huko New Orleans. Kwa Birdman huu ni kama utamaduni wake wa kila mwisho wa mwaka. Mwaka jana Lil Wayne aliungana nae.

Tarehe 22 Nov ya kila mwaka ni siku ya asante duniani, siku ambayo mtu yeyote mwenye kutambua thamani wa mtu mwingine anajiandaa kusema asante kwa mtu huyo au jamii fulani kusema tu kwa mdomo au kutoa chochote kama ishara ya kutambua mchango kwake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels