Pages

Friday, November 30, 2012

Waliomkata vidole na kumuibia vitu Sharo Milionea baada ya ajali wakamatwa.



Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma za kumkata vidole na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya gari na kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa website ya thisisdiamond.com watu hao wamekutwa na vitu alivyokuwa navyo marehemu Sharo Milionea kama vile
T-shirt, Viatu, Simu ya mkononi, Pete, Cheni, Tairi moja la gari , pamoja na Battery la gari ambalo marehemu alipata nalo ajali.

Taarifa za awali zinasema watuhumiwa hao walikuwa sita lakini wamekamatwa wanne hadi sasa, na jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa wawili.

Inasemekana watu hao waliamua kumkata vidole marehemu baada ya kushindwa kumvua pete.
Hata hivyo jeshi la polisi bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na kukamatwa kwa watu hao.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels