Msanii Barnaba Elias ameendelea kuandamwa na mfululizo wa mikosi,
baada ya wikiendi iliyopita kuibiwa gitaa lake ambalo alipewa na Mke wa
Rais wa Marekani aliyopita Mama Laura Bush.
Barnaba alielezea
kusikitishwa na tukio hilo ambapo anasema liliibwa maeneo ya Leaders nje
ya ofisi za THT ambapo ndipo makao makuu ya kituo chao cha kazi.
Barnaba alisema, baada ya kuingia katika ofisi za
THT siku ya jumamosi, majira ya saa kumi na mbili na kufanya mambo yake,
alishangaa kutolikuta gitaa lake hilo alilopewa kama prize Asset na
Laura Bush, Mke wa Rais aliyepita na alichanganyikiwa kidogo kwa namna
lilivyotoweka.
“Ninavyokwambia nilifunga milango yote lakini hawa jamaa wametumia
mbinu kali maana hakuna mtu aliyeshituka.
Barnaba anasema bado juhudi za
kulitafuta gitaa hilo zinaendelea na anasema atashukuru kama atapata
mtu atakayemsaidia kwa taarifa ili kulipata gitaa hilo
0 maoni:
Post a Comment