Pages

Saturday, November 17, 2012

RAPPER QUICK ROCKER AMEANZISHA LEBLE "INAITWA 255"


Rapper wa kundi la Rockers, Abbott Charlesaka Quick Rocker amesema anaanzisha record label yake aliyoipa jina la 255 Ikiwa ni code za nchi Tz .

Rapper huyo anayetamba na ‘club banger’ yake mpya iitwayo ‘Katika’ alisema pia anafungua studio yake ya kurekodi muziki aliyoipa jina la ‘Big Step’.

Quick alidai kuwa studio yake itapatikana maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo hitmaker huyo wa ‘Bullet’ alisema pamoja na kuwa na studio yake mwenyewe, bado ataendelea kufanya kazi na studio zingine na kila aina ya producer ilimradi apate kitu kizuri.

Akiongelea wimbo wake mpya, ‘Katika’, Quick Rocker alieleza kuwa aliamua kutoka tofauti kwakuwa muziki wa Tanzania umebadilika ambapo watu wengi hupenda nyimbo zinazochezeka.

Katika mahojiano hayo, rapper huyo alizungumzia pia uwepo wa kundi lake la Rockers ambalo lilikuwa limevunjika na kudai kuwa kundi hilo limerudi tena na mashabiki wategemee mambo mapya.

0 maoni:

Post a Comment

Labels