Pages

Wednesday, November 21, 2012

RAPPER SAIGON AINGIA KATIKA BIFU NA BIG BOSS ROZAY



Rapper Saigon wa Marekani siku chache zilizopita ametoa tamko katika kituo cha Redio cha Power 105.1 nakusema kuna baadhi ya wasanii ambao wameapa kuwa akikutana nao ni lazima awatie ngumi akidai kuwa mashairi yao yanaharibu watoto kutokana na lugha mbovu zinazo tumiwa katika mashairi yao kwani zinahusisha maswala ya ngono.

Ishu ambayo ilimkela Saigon kuwa mara nyingi akiwaona madogo street wakitiririka mashairi ya Rozay ambayo ni matusi matupu na wanaimba kama ni maneno ambayo yana maadili kwao.

Saigon alimtaja Rozay kuwa ndio anamtamani sana kumdunda na akifuatia 2 chainz ambao wote mashairi yao yanamatusi hayana maadili.


Wakati huo huo Rapper kutoka MMG si mwingine ni Gunplay alipata taarifa za msanii huyo  na akasema, kama Saigon anaweza kumpiga The Big Boss Rozay ajaribu na ataona kitakacho tokea.

0 maoni:

Post a Comment

Labels