Looks like producer mkongwe wa Hip hop, P Funk Majani ambaye watu wengi walifikiri amepotea kwenye ramani ya muziki wa Tanzania,anarudi kwa kishindo cha aina yake baada ya producer huyo machachari kumuingiza katika studio za Bongo Records, msanii Keko kutoka Uganda kushiriki katika Kolabo ambayo itakuwa na si chini ya wasanii wanne.
Rapper huyo mahiri wa Kike kutoka Uganda,aliingia ndani ya booth za studio za Bongo Records, jana mchana na kushiriki katika kolabo ya Wimbo ambayo ndani yake kutakuwa na jumla ya wasanii wanne akiwemo Ay ambaye tayari alishaingiza sauti zake kitambo.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa super producer wa studio hiyo Bwana P Funk Majani au kinywele kimoja, Keko ameshiriki kwenye nyimbo ambayo imepewa jina la No Name ambayo ni tittle ya project ya album yenye jina hilo hilo la No Name.
Kwa mujibu wa majani, ukiachia AY na Keko, ambao tayari wameshaingiza sauti zao, kuna nafasi ya wasanii wawili zaidi ambapo moja kati ya wasanii ambaye P Funk alikuwa anataka awemo katika kolabo hiyo ni msanii Chrstian Bella, ambaye hata hivyo habari zinasema hayupo nchini kwa sasa.
P-Funk alifunguka zaidi na kusema, kama itashindikana kupatikana Christian Bella kwa wakati, basi Wapenzi na wadau wa muziki watume maoni yao ya kumpa nafasi msanii wa kikongo ambaye achukue nafasi ya Christian Bella katika kolabo hiyo.
Kolabo hiyo ni moja ya muendelezo wa project ya No Name ambayo inahusisha vichwa hot vya production na muziki kama Dunga, Lamar, P Funk mwenyewe, Master J na wengineo.
Kwa sehemu kubwa ya siku ya jana Producer P funk Majani, pamoja na swahiba wake Jay Mo walikuwa karibu na msanii huyo kutoka Uganda, waki hang out pamoja, dalili ambayo iliyoonyesha kumkubali sana Rapper huyo.
Tuma maoni yako ya juu ya msanii gani achukue nafasi ya Christian Bella katika nyimbo hiyo.
Na Bongo5
0 maoni:
Post a Comment