Pages

Sunday, November 18, 2012

HEMED SULEIMAN ANADAIWA MILIONI 1



Yule Mkali wa Misifa na Mwenye kuwa na Nick name kibao, HEMED SULEIMAN Maarufu kama "PHD,AMITHA BATCHAN, ALEJANDRO, CASSANOVA, KING WA MALAVI DAVI", amjikuta katika wakati mgumu baada ya kuvuja kwa data kuwa ana deni zaidi ya Shilingi Millioni 1, katika Duka Fulani la Nguo, hapa DSM

Kwa Mujibu wa taarifa kutoka DT, Muuzaji wa Duka hilo maarufu lililopo Kinondoni (Jina Limehifadhiwa), amesema kuwa mwanzo ilikuwa ni kawaida ya CASSANOVA kuchukua mavazi dukani hapo na kulipa.

Aidha jamaa anatiririka kuwa, baada ya Muda kadhaa, PHD alianza kuchukua Nguo kwa Wiki na mpaka hivi sasa anadeni kali lisiloshuka Chini ya Milioni 1.

"Hemedi tunamuamini,lakini sasa hali hii inafikia kuwa vita kwa sababu kiasio cha fedha tunachomdai ni kikubwa kwa sababu watu wanafanyakazi, na wanahitaji kulipwa Mshara. Hivi sasa tunafikiria kuchukua maamuzi ili aweze kutulipa haraka. Jamaa siku hizi haji hapa na wala sijamuona. 

Sasa sielewi anakimbia deni au lah" Alifunguka jamaa Muuza Duka

0 maoni:

Post a Comment

Labels