Muimbaji wa nchini Kenya Nyota Ndogo amekanusha ripoti zilizoenea kuwa ni mjamzito.
Mama huyo wa watoto wawili na mwenye miaka 31 aligeuka kuwa gumzo
kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na madai kuwa anategemea kupata
mtoto wa tatu.
Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Abdallah
alikiambia kituo kimoja cha radio mjini Mombasa kuwa, “Nimenepa tu na
nipo kwenye hatua katika maisha yangu ambapo nimerelax.
Ni mapema mno
kwangu kuwa na mtoto wa tatu. Mtoto wangu wa pili ndio ana miaka miwili
sasa.”
Na;-www.bongo5.com
0 maoni:
Post a Comment